• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Uholanzi

    (GMT+08:00) 2018-04-10 19:22:58

    Rais Xi Jinping wa China leo huko Boao amekutana na waziri mkuu wa Uholanzi Bw. Mark Rutte.

    Rais Xi amesema utandawazi unaendana na maslahi ya pamoja ya nchi zote, ambazo zinapaswa kuzoea utandawazi badala ya kusitisha hatua zao kutokana na changamaoto au matatizo ya muda. Ameongeza kuwa nchi zote zinapaswa kushikilia mtazamo wazi wa maendeleo na kufanya mafungamano ya kiuchumi yawe na uwazi, ujumuishi, na uwiano zaidi ili yanufaishe binadamu wote.

    Bw. Rutte amesema Uholanzi inatilia maanani kazi muhimu zinazofanywa na China kwenye mambo ya kimataifa, pia inaunga mkono biashara huria, na kufanya juhudi kuhimiza uhusiano kati ya Ulaya na China.

    Rais Xi pia kwa nyakati tofauti amekutana na mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bibi Christine Lagarde anayehudhuria mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Boao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako