• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Uingereza wapongeza mazungumzo ya 10 kati ya vyama vya kisiasa vya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-04-10 19:35:57

    Mazungumzo ya awamu ya 10 kati ya vyama vya kisiasa vya China na Uingereza yamefanyika hapa Beijing.

    Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May wametoa barua za pongezi kwa mazungumzo hayo kwa nyakati tofauti. Rais Xi amesema, tangu mazungumzo ya vyama vya kisiasa kati ya nchi hizo mbili yafanyike katika miaka kumi iliyopita, vyama vya siasa na wanasiasa kutoka nchi hizo mbili wamefanya mazungumzo ya kina kuhusu ajenda zinazofuatiliwa na pande mbili. Mazungumzo hayo yametoa mchango katika kuzidisha maelewano na uaminifu wa pande mbili na kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na yamekuwa sehemu muhimu inayounda mfumo wa mawasiliano kati ya nchi hizo mbili.

    Bibi May amesema, mwaka huu ni mwaka muhimu kwa uhusiano kati ya China na Uingereza, uhusiano huo utaimarika katika zama za dhahabu, na kupata uhai mpya kwa kuelekea uhusiano wa kimkakati na kiwenzi wa pande zote wa dunia katika karne 21, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuzidi kuimarisha uhusiano huo kwa pande zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako