• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yamkamata mtaalamu wa mabomu wa kundi la Boko Haram

    (GMT+08:00) 2018-04-11 08:28:36

    Jeshi la Nigeria limethibitisha kuwa vikosi vyake vimekamata mshukiwa wa ugaidi mwenye utaalamu wa kutengeneza mabomu ya kienyeji kwa ajili ya kundi la kigaidi la Boko Haram. Msemaji wa jeshi hilo Bw. Onyema Nwachukwu amesema mshukiwa huyo anayetambulika kwa jina la Adamu Hassan alikamatiwa katika jimbo la Gombe lililoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kufuatia operesheni ya pamoja ya jeshi na polisi wa siri iliyofanyika jumatatu. Msemaji huyo pia amesema mshukiwa huyo amekiri makosa kwa mamlaka ya usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako