• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wasema kufanikiwa kwa uchaguzi mkuu DRC ni muhimu kwa amani ya maziwa makuu

    (GMT+08:00) 2018-04-11 08:43:02

    Umoja wa mataifa umesema uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufanyika kwa mafanikio ni hatua muhimu ya kuhimiza amani na utulivu kwenye eneo la maziwa makuu.

    Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa kwenye eneo la maziwa makuu Bw Said Djinnit amesema uchaguzi unaoaminika na shirikishi, ukifuatiwa na makabidhiano ya madaraka kwa amani, vitakuwa na manufaa kwa amani, utulivu na maendeleo ya eneo la maziwa makuu.

    Akiongea kwenye mkutano wa Umoja wa mataifa unaofuatilia maendeleo ya kikanda ikiwa ni pamoja na maswala ya kibinadamu na makundi yenye silaha, Bw Djinnit amelitaka baraza la usalama kuendelea kuwa na sauti moja kwenye uungaji mkono wa utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa mwezi Desemba mwaka 2016, kwamba uchaguzi wa rais utafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako