• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yataka aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Sudan Kusini azuiliwe kushiriki kwenye mazungumzo ya amani

    (GMT+08:00) 2018-04-11 08:53:11

    Sudan Kusini imehimiza jumuiya ya kimataifa kumzuia aliyekuwa mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Bw Paul Malong kushiriki kwenye duru ya tatu ya mazungumzo ya amani yanayoendeshwa na viongozi wa kikanda.

    Msemaji wa rais wa Sudan Kusini Bw. Ateny Wek Ateny, amesema Bw Malong alikuwa fisadi na mvuruga amani, ambaye hatakiwi kuwa na nafasi kwenye mazungumzo yajayo ya amani yanayoendeshwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) nchini Ethiopia.

    Bw Ateny pia amesema ikulu ya Sudan inakanusha madai yote ya Bw. Malong dhidi ya rais. Pia imehimiza Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutotambua nafasi zote za Bw. Malong kutokana na kusababisha mgogoro wa kisiasa nchini humo akiwa serikalini tangu mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako