• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasisitiza kuiunga mkono Sudan katika kutimiza utulivu

    (GMT+08:00) 2018-04-11 09:01:49

    Naibu wa rais wa Kenya Bw. William Ruto amesisitiza uungaji mkono wa nchi yake kwa Sudan katika kutimiza amani na utulivu, na kuandaa katiba ya kudumu ya nchi hiyo.

    Bw. Ruto ambaye yuko kwenye ziara ya siku tatu nchini Sudan amesema hayo jana baada ya kukutana na Rais Omar al-Bashir wa Sudan.

    Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano huo, Bw. Ruto amesema Kenya itaunga mkono serikali ya Sudan, rais al-Bashir na wananchi wa Sudan, katika kazi ya kuandika katiba mpya. Ameongeza kuwa Kenya inajaribu kuiga uzoefu wa Sudan kwenye sekta ya kilimo na uzalishaji wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako