• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Syria yalialika OPCW kufanya uchunguzi mjini Douma

    (GMT+08:00) 2018-04-11 09:25:10

    Wizara ya mambo ya nje ya Syria imetoa taarifa kuwa serikali ya Syria imelialika rasmi Shirika la kupiga marufuku silaha za kikemikali OPCW kutuma ujumbe wa uchunguzi kuingia mjini Douma kwenye eneo la Ghouta Mashariki, na kuchunguza madai ya shambulizi la kikemikali lililotokea Aprili 7 mjini humo.

    Hatua hiyo imechukuliwa kujibu kashfa ya nchi kadhaa za magharibi dhidi ya serikali ya Syria. Taarifa pia imesema serikali ya Syria inalaani vikali vitendo vya kutumia silaha za kikemikali katika hali yoyote na sehemu yoyote, na imeahidi kuwa itatoa msaada wote unaohitajika kwa ujumbe wa uchunguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako