Juzi video kuhusu mdunguaji wa jeshi la Israel kumfyatulia risasi mpalestina ilisambaa kwenye mtandao wa Internet, ikionyesha mdunguaji mmoja akimfyatulia risasi mpalestina aliyekuwa karibu na uzio wa mpaka kati ya Israel na Gaza, , na askari wa jeshi la Israel waliokuwepo walionekana kushangilia baada ya kuona mpalestina huyo akianguka kutokana na kujeruhiwa na risasi.
Msemaji wa jeshi la Israel amesema video hiyo ilipigwa mwezi Desemba mwaka jana kwenye ukanda wa Gaza. Askari hao kwenye video wataadhibiwa, na jeshi la Israel litachunguza tukio hilo kwa pande zote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |