• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Tanzania nchini China asema China inaonesha busara kubwa kwa kufungua mlango zaidi

    (GMT+08:00) 2018-04-11 10:05:41

    Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki amesema, China imekuwa ikiongeza nguvu katika kufungua mlango, hali ambayo imetoa mchango mkubwa kwa utandawazi na biashara huria, na kuonesha busara ya nchi kubwa.

    Katika mahojiano hayo, Bw. Kairuki alieleza wasiwasi kwamba kupamba moto kwa mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani kunaweza kuathiri maendeleo ya uchumi duniani, akiona kuwa hatua ya Marekani ya kutoza ushuru mkubwa wa forodha kwa bidhaa za China, itaathiri makundi hayo makubwa ya uchumi duniani, na pia italeta hatari kwa maendeleo ya uchumi ya pande zinazohusika za biashara duniani.

    Amesema, "ukweli ni kwamba mgogoro huu wa kibiashara hauna manufaa kwa taifa lolote na ulimwengu kwa ujumla, ukiachwa uendelee utakuwa na athari kubwa kwenye utaratibu wa kimataifa wa biashara…. mtazamo wa sasa wa serikali ya Marekani ni kuangalia ndani, masoko yao na mambo yao wenyewe, Marekani ikitetereka, uchumi wa dunia ukitetereka maana yake hata fursa, na uwekezaji utaathirika……utandawazi una manufaa kwa pande zote, unatoa fursa kwa mataifa yote, ni utandawazi unaotoa fursa kwa mataifa yote, lakini kweli kuna kazi za kufanya kwa kila upande, mfumo wa dunia lazima uendane na mazingira ya sasa na uzingatie maslahi ya watu walio nyuma ile waje mbele…tunategemea kuwa China ambayo sasa inaonekana kuwa mbele duniani katika maswala mbalimbali, itasaidia kusukuma na kuziwezesha nchi za Afrika zinufaike. Kuna mpango wa ushirikiano kwenye kuhimiza uwezo wa uzalishaji ili kuzijengea uwezo nchi za Afrika kuzalisha vitu vya kwenda kwenye soko la kimataifa …..China inafungua fursa zaidi kwa nchi za nje ni wazo jema, toka mwaka 2001 imejiunga na WTO inakuwa inafuata sheria na kanuni za shirika hilo, wanafungua masoko na kulegeza masharti ya uwekezaji kutoka nje kuingia kwenye soko la China hii ni fursa kwa nchi za nje. Mwezi Novemba mwaka huu China imeitisha maonyesho ya kwanza ya kimataifa kwa ajili ya makampuni ya nje kuonesha bidhaa zao katika soko la China, hii inadhihirisha dhamira njema ya China kutaka kufungua soko lake. Sisi Afrika na Tanzania tutachangamkia fursa hii, kutangaza utalii, na kutangaza Tanzanite na bidhaa za Tanzania zenye ubora.

    Bw. Kairuki ameeleza kuwa, hivi karibuni nchi 44 za Afrika zimesaini makubaliano ya eneo la biashara huria, na kupiga hatua kubwa kwa mafungamano ya kiuchumi barani Afrika, lakini wakati huo huo baadhi ya nchi zinatekeleza hatua za upande mmoja na kujilinda kibiashara. Kutokana na hali hii ya kimataifa, msukumo wa China katika kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia na utandawazi umeonesha umuhimu mkubwa zaidi.

    Rais Xi Jinping wa China ameeleza katika hotuba yake aliyoitoa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa mwaka 2018 wa Baraza la Asia la Boao kuwa, sera ya mageuzi na kufungua mlango ya China si kama tu imebadilisha China bali pia imekuwa na manufaa kwa dunia, na imefungua ukurasa mpya wa kuimarisha mawasiliano na maendeleo kati ya China na dunia. Bw. Kairuki amesema, mlango wa China unafunguliwa siku hadi siku, na uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya pande hizo mbili unakuwa na manufaa kwa kwa pande hizo mbili siku hadi siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako