• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya rais Xi Jinping wa China kwenye Baraza la Asia la Boao yakaribishwa na viongozi wa nchi mbalimbali

    (GMT+08:00) 2018-04-11 10:06:40

    Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba katika Mkutano wa Baraza la Asia la Boao, akiahidi kupanua ufunguaji mlango na kukuza ustawi wa dunia. rais Xi Jinping amesisitiza kuwa mageuzi na ufunguaji mlango wa China vinalingana na matumaini ya wananchi ya kupata maendeleo, kufanya uvumbuzi na kuishi maisha mazuri. Pia inalingana na mwelekeo wa dunia wa kutafuta maendeleo, ushirikiano na amani.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres alisema pendekezo la China la "Ukanda mmoja, Njia moja" linaweza kuchangia kuifanya dunia iwe na haki, amani na ustawi zaidi. Pia amekubaliana na rais Xi kuwa utandawazi ni mkondo usiozuilika.

    Rais Alexander Van der Bellen wa Austria amesema sera ya China ya mageuzi na kufungua mlango imepata mafanikio makubwa, akiongeza kuwa China itashikilia njia hiyo na itawanufaisha China na washirika wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako