• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq kuchukua hatua ili kuzuia kundi la IS kufanya shambulizi la kuvuka mpaka kutoka Syria

    (GMT+08:00) 2018-04-11 17:33:11

    Waziri mkuu wa Iraq Bw. Haider al-Abadi amesema, Iraq itachukua hatua zote za lazima ili kuzuia kundi la IS lililopo nchini Syria kufanya shambulizi la kuvuka mpaka.

    Bw. al-Abadi amesema, kundi la IS bado lipo sehemu ya mashariki ya Syria iliyoko karibu na mpaka wa Iraq, na serikali ya nchi hiyo itachukua hatua zote za lazima kukabiliana na tishio la wapiganaji wa kundi hilo na kulinda raia wake. Pia amesema, serikali ya Iraq itashirikiana na Syria na Russia kuwaangamiza wapiganaji wa kundi hilo waliopo mashariki mwa Syria, huku akiongeza kuwa Iraq haikusudii kuingilia mambo ya ndani ya Syria na hatima ya Syria inatakiwa kuamuliwa na wananchi wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako