• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alaani mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

    (GMT+08:00) 2018-04-11 17:50:22

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya askari wa kulinda amani kutoka Rwanda na kujeruhiwa kwa askari wengine nane wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu huyo imesema, tukio hilo lilitokea mjini Bangui hapo jana wakati wa majibizano ya risasi kati ya kikosi hicho na makundi yenye silaha baada ya operesheni ya pamoja na jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati ya kuwaondoa makundi ya waasi yenye silaha.

    Bw. Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, na pia kwa serikali ya Rwanda, na kuwatakia majeruhi kupona upesi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako