• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China alitaka Baraza la Asia la Boao kusaidia kuendeleza ustawi wa pamoja

    (GMT+08:00) 2018-04-11 17:50:44

    Rais Xi Jinping wa China amelitaka Baraza la Asia la Boao (BFA) kuendelea kuunga mkono maendeleo ya China na kuchukua nafasi zaidi katika kuendeleza ustawi wa pamoja duniani.

    Rais Xi amesema hayo leo alipokutana na wajumbe wa sasa na wajao wa Bodi ya Wakurugenzi wa BFA mkoani Hainan hapa China. Amesema kama nchi mwenyeji wa mkutano wa Baraza hilo, China itatoa nafasi pana ya maendeleo kwa Baraza hilo, huku Baraza hilo likiweka mzizi wake Asia na kulihudumia bara hilo.

    Rais Xi ameongeza kuwa, Baraza hilo linapaswa kuwa wazi na jumuishi na kupata maendeleo kutokana na msukumo wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako