• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Afrika ya China na Jamhuri ya Kongo yazindua jengo jipya la ofisi nchini Jamhuri ya Kongo

    (GMT+08:00) 2018-04-11 20:08:01

    Hafla ya kuzindua ofisi mpya ya Benki ya Afrika ya China na Jamhuri ya Kongo iliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Kilimo ya China na serikali ya Jamhuri ya Kongo imefanyika katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Brazzaville.

    Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Fedha na Bajeti wa Jamhuri ya Kongo Bw. Calixte Nganongo amesema, Benki hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015, ni mojawapo ya mafanikio muhimu ya ushirikiano kati ya China na Jamhuri ya Kongo.

    Kwa upande wake, naibu gavana wa Benki ya Kilimo ya China Bw. Guo Ningning amesema Benki ya Afrika ya China na Jamhuri ya Kongo ni ya kwanza inayofadhiliwa na Benki ya Kilimo ya China barani Afrika. Ameongeza kuwa, kuanzishwa kwake kutaleta faida kubwa katikati ya Afrika na kutoa mchango kwa maendeleo ya kiuchumi ya Jamhuri ya Kongo na ushirikiano kati ya China na nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako