• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya ndege ya jeshi nchini Algeria yafikia 257

    (GMT+08:00) 2018-04-11 20:10:25

    Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya ndege ya jeshi iliyoanguka mapema leo katika uwanja wa ndege wa jeshi wa Boufarik mkoani Blida, kusini magharibi mwa mji mkuu wa Algeria, Algiers imefikia 257.

    Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imethibitisha kuwa, ndege hiyo ilianguka kandokando ya kambi ya jeshi la anga ya Boufarik mkoani humo.

    Habari zinasema, ndege hiyo iliyokuwa na wanajeshi zaidi ya 250, ilikuwa ikielekea mkoa wa kusini magharibi wa Bechar kabla ya kuanguka.

    Mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Ahmed Gaid Salah ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu na kutaka uchunguzi wa wazi kuhusu tukio hilo ufanyike.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako