• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump atoa shukrani kwa madhumuni mengine

    (GMT+08:00) 2018-04-11 20:16:35

    Rais Xi Jinping wa China jana alitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa baraza la Asia la Boao, ambayo imeeleza hatua na sera muhimu za kuzidisha mageuzi na ufunguaji wa mlango. Hotuba hiyo imepongezwa na jumuiya ya kimataifa, na rais Donald Trump wa Marekani pia ametoa taarifa kupitia mtandao wa kijamiiakishukuru rais Xi kwa hotuba yake.

    Baada ya kutishia kuanzisha vita vya kibiashara dhidi ya China, rais Trump sasa anaonekana kutoa taarifa chanya kwa madhumuni mengine, na kutokana na shinikizo la dunia, anapaswa kuonesha msimamo wa kirafiki. Jumuiya ya kimataifa inaona kuwa hotuba ya rais Xi imeonesha tena majukumu ya China kwa dunia. Wakati China ikiwa mlinzi wa biashara huria ya dunia na mfumo wa biashara wa pande nyingi, serikali ya Marekani inapaswa kutoa jibu chanya.

    Aidha, rais Trump anatoa shukrani kwa hatua ya ufunguaji mlango ya China katika sekta ya ushuru, magari na hakimilili za ubunifu ili kuipotosha jumuiya ya kimataifa kuwa China imesalimu amri katika mvutano wa kibiashara kati yake na Marekani.

    Mbali na hayo, rais Trump anatoa shukrani kwa ajili ya siasa ya ndani. Hivi sasa serikali ya Trump inakabiliwa na shinikizo kubwa la ndani, na imechukua uamuzi wa kuanzisha vita ya kibiashara na China ili kuwafariji wananchi na kuondoa sauti za kukosoa. Shukrani yake inalenga kupeleka habari kwa wananchi kwamba sera ya serikali ya Trump imefanikiwa, China imesalimu amri katika mvutano huo. Kuanzisha vita ya biashara na China ni njia moja ya Marekani kuzuia maendeleo ya China na kulinda hadhi yake ya uongozi duniani. Lakini China sio tu itaendelea kuhimiza mageuzi na ufunguaji wa mlango, bali pia itafanya juhudi kushinda katika vita hivyo vya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako