• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufunguaji mlango wa China hauamuliwi na nchi nyingine

    (GMT+08:00) 2018-04-11 20:19:02

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, hatua muhimu zilizotangazwa na China kuhusu kupanua ufunguaji mlango hazihusiki na mgogoro wa biashara wa sasa kati ya China na Marekani.

    Amesema hatua hizo za China haziathiriwi na nchi nyingine, na nchi nyingine pia hazina uwezo wa kuilazimisha China kuchukua hatua hizo, na kwamba China siku zote inasisitiza kuwa ufunguaji mlango ni sera ya kitaifa ya muda mrefu, na kushikilia ujenzi wa taifa kwa kufungua mlango. Pia amesema China kutangaza hatua hizo ni muhimu kwa kutekeleza yaliyomo kwenye ripoti ya Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China na ripoti ya kazi ya serikali, ni hatua muhimu zinazochukuliwa na China kutokana na mahitaji yake, ajenda yake na mpango wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako