• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Trilioni 13 zahitajika kujenga miundombinu kwenye sekta ya elimu

  (GMT+08:00) 2018-04-11 20:40:36

  Serikali ya Tanzania imelieleza Bunge kuwa inahitaji Sh trilioni 13 kumaliza changamoto ya ujenzi wa miundombinu kwenye sekta ya elimu.

  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda amesema kiasi hicho kimefahamika baada ya serikali kukokotoa.

  Kakunda alikuwa anamjibu Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) ambaye katika swali la nyongeza, alihoji ni kwa nini serikali isitenge fungu maalumu ikiwa ni pamoja na kukopa ili kuondokana na kero katika elimu.

  Kakunda amesema, Serikali inatambua kuna uhaba wa nyumba za walimu katika shule za msingi na sekondari na ndiyo maana imekuwa ikijitahidi kila mwaka kuzijenga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako