• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Standard Chartered kutumia Sh44.8 trilioni kuwawezesha wafanyabiashara wanaokwenda China

  (GMT+08:00) 2018-04-11 20:40:57

  Benki ya Standard Chartered inatarajia kutumia Sh44.8 trilioni kuwawezesha wafanyabiashara wanaokwenda China, ili kuimarisha biashara kati ya taifa hilo na Afrika.

  Fedha hizo zitakopeshwa kwa wafanyabiashara hao kuanzia sasa mpaka mwaka 2020, ikiwa ni sehemu ya mpango wa China kukuza ushirikiano na Tanzania chini ya utekelezaji wa One Belt One Road Initiative.

  Mpango huo ulibainishwa na mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo nchini, Sanjay Rughani alipokutana na wateja Wachina waliopo nchini kuwaeleza ushiriki wa Standard Chartered katika utekelezaji mpango huo wa Rais Xi Jinping ulioanzishwa mwaka 2013.

  Naye mkurugenzi wa maendeleo ya uwekezaji Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristides Mbwasi kwa niaba ya waziri mwenye dhamana, alisema elimu inahitajika kwa wafanyabiashara kuelewa fursa zilizopo katika mpango huo wajipange kunufaika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako