• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Watengenezaji saruji Uganda watakiwa kupunguza bei

  (GMT+08:00) 2018-04-11 20:41:18

  Wizara ya biashara na vyama vya ushirika nchini Uganda imetishia kukubalia saruji ya bei rahisi kuingizwa nchini humo iwapo watengenezaji wa bidhaa hiyo hawatapuguza bei.

  Waziri wa biashara Amelia Kyambadde amewapa watengenezaji wa saruji nchini humo muda wa wiki tatu kupunguza bei zao.

  Kwa sasa mfuko mmoja wa saruji umeongezeka bei kwa kati ya shilingi 5,000 na 11,000 ndani ya mwezi mmoja na hivyo kusababisha mzozo kwenye sekta ya ujenzi.

  Kampuni mbili kuu za kuzalisha saruji Tororo na Hima Cement ambazo huzalisha asilimia 80 ya bidhaa hiyo zimesema ongezeko la bei limesababishwa na kupungua kwa umeme na hivyo hawawezi kuzalisha kwa wingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako