Baraza la usalama la Umoja wa mataifa halijapitisha miswada mitatu ya azimio iliyowasilishwa na Marekani na Russia kuhusu utaratibu wa uchunguzi juu ya shambulizi la kikemikali nchini Syria. Naibu balozi wa China katika Umoja wa mataifa Bw. Wu Haitao amesema baraza la usalama linapaswa kudumisha mshikamano, kufanya baraza hilo na Shirika la kupiga marufuku silaha za kikemikali OPCW kuwa njia kuu ya kushughulikia suala la silaha za kikemikali la Syria, na kutatua masuala yaliyopo kwa uratibu na kwa hatua mwafaka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |