• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi ya Mabingwa Ulaya: Dakika za nyongeza zaipeleka Real Madrid nusu fainali

  (GMT+08:00) 2018-04-12 08:29:49

  Goli la penati lilofungwa na Cristiano Ronaldo katika dakika za majeruhi limeipeleka Real Madrid katika nusu fainali za ligi ya mabingwa Ulaya.

  Penati hiyo ilikuja baada ya Medhi Benatia kumdondosha Lukas Vazquez kwenye eneo la hatari.

  Mchezo huo ulimalizika kwa kwa Juventus kupata ushindi wa magoli 3-1 lakini wametolewa katika michuano hiyo kwa aggregate ya jumla ya magoli 4-3.

  Bayern Munich nao wametinga nusu fainali baada ya kumaliza mechi yao dhidi ya Sevilla kwa matokeo ya bila kufungana lakini wakiwa na magoli 2 kibindoni dhidi ya 1 la Sevilla katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

  Sasa Real Madrid inaungana na Liverpool, Roma na Bayern katika droo ya timu nne zilizosalia, droo itafanyika Nyon, Uswisi Ijumaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako