• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yalaani azimio la serikali ya Marekani kuhusu hali ya kibinadamu nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-04-12 08:43:12

    Serikali ya Ethiopia imesema azimio lililopitishwa hivi karibuni na baraza la chini la bunge la Marekani kulaani rekodi ya haki za binadamu ya utawala bora nchini Ethiopia., limekuja katika wakati usiofaa.

    Azimio hilo limeitaka serikali ya Ethiopia kuondoa hali ya hatari, kuacha matumizi ya nguvu kupita kiasi, kuchunguza mauaji na matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano makubwa yaliyotokea katika majimbo ya Oromia na Amhara. Azimio hilo pia limeitaka serikali ya Ethiopia iwaachie wapinzani, wanaharakati na waandishi wa habari waliokamatwa wakitekeleza haki yao ya kikatiba.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema azimio hilo rahisi halisaidii na linakwenda kinyume na urafiki uliopo kati ya Marekani na Ethiopia. Taarifa hiyo pia imesema azimio hilo haliendani na hali halisi nchini Ethiopia, na imepuuza mafanikio yaliyopataikana hivi karibuni nchini Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako