• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yaanza mchakato wa majadiliano kuhusu eneo la biashara huria

    (GMT+08:00) 2018-04-12 08:43:33

    Serikali ya Zambia imeanzisha mjadala wa ngazi ya juu kuhusu eneo la biashara huria la Afrika AfCFTA ili kuiwezesha nchi hiyo kuwa na msimamo wa pamoja kabla ya kusaini makubaliano hayo.

    Waziri wa biashara na viwanda wa Zambia Bw Christopher Yaluma amesema Zambia inatambua kuwa makubaliano hayo yataipatia soko kubwa na kuongeza nafasi za ajira, lakini haitasaini makubaliano hayo kabla ya kufanya mazungumzo shirikishi na wadau wote.

    Waziri wa mambo ya nje wa Zambia Bw. Joseph Malanji amesema Zambia imefanya majadiliano kwenye vipengele vinavyohusu bidhaa, huduma na utatuzi wa migogoro, lakini vipengele vingine vinavyohusu ushindani wa kibiashara, uwekezaji na hataza bado havijajadiliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako