• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda na DRC zasaini makubaliano ya kuhimiza biashara

    (GMT+08:00) 2018-04-12 08:52:26

    Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC zimesaini makubaliano ya kuondoa vizuizi visivyo vya ushuru kwa ajili ya kuhimiza biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Makubaliano hayo yamefikiwa jana wakati waziri wa biashara wa Uganda Bibi Amelia Kyambadde alipokutana na waziri wa biashara ya nje wa DRC Bw Jean-Lucien Bussa Tongba huko Kasese nchini Uganda.

    Taarifa ya pamoja iliyosainiwa na mawaziri hao wawali imesema makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo, yanalenga kuimarisha usimamizi wa vigezo na ubora wa bidhaa, na mabadilishano ya habari na takwimu. Bidhaa nyingi zaidi zinatarajiwa kupewa ruhusa ya kuvuka mpaka wa nchi hizo mbili.

    Taarifa pia imesema mawaziri hao wamepitisha orodha ya bidhaa zitakazonufaika na Mfumo wa kurahisisha biashara STR, ambao utawanufaisha wafanyabiashara wadogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako