• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Kenya zaahidi kushirikiana kutatua masuala ya usalama ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-04-12 09:47:50

    Sudan na Kenya zimesisitiza ahadi yao ya kushirikiana kutatua masuala ya usalama barani Afrika hasa nchini Sudan Kusini.

    Taarifa hiyo imetolewa baada ya makamu wa rais wa Sudan Bw Bakri Hassan Saleh kuzungumza na naibu wa rais wa Kenya Bw William Ruto akiwa ziarani nchini humo. Pande hizo mbili zimejadiliana kuhusu hali ya kikanda, na kukubaliana kutoa mchango wa pamoja katika kutafuta utatuzi wa kudumu.

    Bw. Saleh pia amesema, Sudan itaendelea kushirikiana na Umoja wa Afrika na mashirika yake kudumisha utulivu wa kikanda.

    Bw. Ruto amezihimiza nchi za Afrika kutoa mchango zaidi kwenye mchakato wa amani wa Somalia na Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako