• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wa China na Iran watoa mwito wa kutekelezwa kwa makini kwa makubaliano ya nyuklia ya Iran

    (GMT+08:00) 2018-04-12 12:57:40

    Kongamano la ushirikiano wa sekta ya nishati ya nyuklia kati ya China na Iran lilifanyika jana hapa Beijing, watu waliohudhuria kongamano hilo wamesema makubaliano ya nyuklia ya Iran hayakupatikana kwa urahisi, na kutoa mwito kwa pande zote husika kuendelea kutekeleza makubaliano hayo kwa makini na kwa ufanisi.

    Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano huo, naibu mkurugenzi wa Shirika la nishati ya atomiki la China Bw. Wang Yiren alisema kufikiwa kwa makubaliano ya nyuklia ya Iran ni mfano wa kutatua masuala ya kimataifa kwa njia ya amani, na kulinda ukamilifu na heshima ya makubaliano hayo kuna umuhimu mkubwa katika kuimarisha mfumo wa kutoeneza silaha za nyuklia duniani, na kuhimiza maendeleo ya matumizi ya nishati ya nyuklia kwa njia ya amani. .

    Naibu mwenyekiti wa Shirika la nishati ya atomiki la Iran amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran yanasaidia kuihimiza Iran kufanya ushirikiano wa nishati ya nyuklia na nchi mbalimbali kwa njia za wazi, na hivi sasa yamepata mafanikio. Amesema kazi muhimu kwa sasa ni kuhakikisha ukamilifu na ufanisi wa makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako