• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la Houthi lasema limerusha makombora dhidi ya maeneo kadhaa ikiwemo wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2018-04-12 16:54:20

    Kundi la Houthi la Yemen limesema, limerusha makombora dhidi ya maeneo kadhaa yaliyolengwa ikiwemo wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia na kampuni ya mafuta ya Aramco.

    Taarifa iliyotolewa na kundi hilo kupitia Shirika la Habari la Saba la Yemen imesema, makombora hayo yamelenga wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia huko Riyadh na makombora mengine dhidi ya kampuni ya mafuta ya Aramco huko Najran na mji wa Mfalme Abdullah mkoani Gizan nchini Saudi Arabia.

    Upande wa Saudi Arabia umesema, kikosi cha ulinzi wa anga cha nchi hiyo kimezuia makombora yaliyorushwa na kundi la Houthi huko Riyadh na Najran na kuangusha ndege isiyo na rubani ya kundi hilo huko Gizan. Mpaka sasa hakuna ripoti yoyote kuhusu vifo au majeruhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako