• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi maalum vya jeshi vya Afrika na washirika kutoka magharibi waanza zoezi la kijeshi nchini Burkina Faso

    (GMT+08:00) 2018-04-12 17:20:16

    Vikosi maalum vya jeshi vya Afrika kutoka nchi za Mali, Mauritania, na Burkina Faso na washirika wao kutoka nchi za Magharibi wameanza zoezi la kijeshi nchini Burkina Faso, ikiwa ni sehemu ya zoezi la kila mwaka liitwalo "Flintlock".

    Zoezi hilo, linalolenga kuimarisha mafunzo na uwezo wa vikosi hivyo maalum katika mapambano dhidi ya ugaidi, linahusisha mbinu za mapigano ya karibu, kuzima moto, na operesheni za anga.

    Mafunzo hayo ya wiki mbili yanayofanyika katika maeneo mbalimbali Afrika Magharibi, yanajumuisha jumla ya askari 1,900 kutoka nchi 20 za Afrika na za Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako