• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mdau wa biashara wa Marekani asema Marekani itaumia yenyewe kama inatekeleza sera ya kujilinda kibiashara

  (GMT+08:00) 2018-04-12 17:23:18

  Baada ya rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kuongeza ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China kwa mujibu wa uchunguzi wa kipengele cha 301 cha Sheria ya Biashara ya Marekani, na kuweka vizuizi kwa China kusafirisha teknolojia na kununua makampuni, Bw. Peter Reisman mwenye uzoefu wa miaka mingi wa uwekezaji kati ya Marekani na China anasema uchunguzi huo hauna msingi wa hali halisi, na Marekani itajiumiza yenyewe kama inatekeleza sera ya kujilinda kibiashara.

  Bw. Reisman amesema uchunguzi wa kipengele cha 301 unaochukuliwa kama ni sababu ya kuongeza ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa za China hauna msingi wa kisheria na hali halisi.

  "Shutuma za rais Donald Trump dhidi ya makampuni ya China katika sekta ya hakimiliki ya ubunifu hazina msingi wowote wa hali halisi. Makampuni ya China kununua makampuni katika nchi za nje kwa kutaka kusafirishwa kwa hakimili ya ubunifu ni hatua inayoamriwa na soko, na inahudumia maendeleo ya uchumi wa China, upanuzi wa matumizi ya wateja wa China, ubunifu wa kujitegemea wa China na matakwa ya maendeleo ya makampuni ya China nje ya China. China ni nchi ya pili duniani kiuchumi, na ni jambo la kawaida kwa makampuni ya China kununua makampuni ya kigeni, sio tu yanataka kuinua ubora wa bidhaa zao, na kuhimiza kuinuka kwa kiwango cha uzalishaji wa ndani ya China, bali pia yanataka kujiongezea ushindani wa kimataifa."

  Amesema kama Marekani inaweka vizuizi kwa uwekezaji na makampuni ya China nchini Marekani, basi Marekani itapata hasara.

  "Kuizuia China kuwekeza nchini Marekani hakuna manufaa kwa uchumi wa kikanda wa Marekani na suala la ajira. Katika miaka ya hivi karibuni, uwekezaji wa makampuni ya China nchini Marekani umeongezeka kwa kasi na kufikia dola za kimarekani bilioni 100, na uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Marekani na China umeunga mkono watu milioni 2.6 wa Marekani kupata kazi kwa njia ya moja kwa moja au isiyo moja kwa moja. Kuweka vizuizi kwa makampuni ya China nchini Marekani au uwekezaji wa China nchini humo sio tu kutaathiri makampuni ya China, bali pia makampuni ya Marekani na hata maendeleo ya dunia."

  Bw. Reisman pia amesema Marekani inapaswa kupanua njia za ushirikiano na China na kutumia mbinu inayofaa kupunguza pengo la kibiashara kati yake na China.

  "Suala la urari mbaya linaloikabili Marekani sio jipya kati ya biashara kati ya China na Marekani. Tokea mwaka 1976, Marekani inakabiliwa na suala hilo katika biashara kati yake na nchi nyingi duniani. Sababu kuu ni kuwa mahitaji ya ndani ya Marekani ni makubwa kuliko utoaji. Pili dola ya Marekani ni sarafu ya akiba duniani, na Marekani ikiwa nchi inayotoa sarafu ya akiba duniani, haina budi kuvumilia urari mbaya katika biashara kati yake na nchi nyingine ili kutoa sarafu, na kuepusha mfumo wa fedha duniani usimame."

  Bw. Reisman amesema Marekani na China zitapata mafanikio kwa pamoja kama zinashirikiana na anaona kuwa pande hizo mbili zinapaswa kufanya mazungumzo kutatua mgogoro wa kibiashara kati yao, kuongeza kasi ya mazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara ya pande mbili kati ya China na Marekani, kusukuma mbele matumizi ya sarafu ya China RMB nchini Marekani, kupanua ushirikiano wa pande mbili katika sekta ya ujenzi wa miundombinu, nishati na akili bandia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako