• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Hewa safi" ya China kuifanya makampuni ya kigeni kupata fursa nyingi zaidi

    (GMT+08:00) 2018-04-12 18:48:28

    Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Boao, ambapo ametangaza hatua nne muhimu za kuendelea kuzidisha ufunguaji mlango, ikiwemo kutoa mazingira ya uwekezaji yenye mvuto zaidi.

    Rais Xi alifananisha mazingira ya uwekezaji kuwa hali ya hewa, akisema "hewa safi inaweza kuvutia zaidi mitaji ya kigeni". Hii inamaanisha kuwa kuboresha mazingira ya uwekezaji kuna umuhimu mkubwa sio tu kwa ufunguaji mlango wa China, bali pia kwa nchi mbalimbali duniani.

    Serikali ya China siku zote inatilia maanani katika ujenzi wa mazingira ya uwekezaji. Katika miaka arobaini iliyopita, uchumi wa China umetimiza maendeleo ya kihistoria, na uzoefu muhimu ni kushikilia ufunguaji wa mlango na kutumia fursa ya mafungamano ya kiuchumi, kujitahidi kushiriki kwenye mgawanyo wa viwanda vya kimataifa na kujenga mfumo kamili wa viwanda. Mitaji ya kigeni pia imetoa mchango mkubwa katika mchakato huo, na kampuni za kigeni zimekuwa sehemu muhimu zinazounda uchumi wa China.

    Uzoefu wa China kuhusu ufunguaji wa mlango umethibitisha kuwa kujenga na kulinda mazingira ya ushindani wenye usawa ni muhimu katika kutoa mazingira ya uwekezaji yenye mvuto zaidi. Miaka ya hivi karibuni, China imesisitiza mfumo wa utawala wa sheria, na kutunga sheria na sera zenye usawa na uwazi, kulegeza masharti ya kuingia kwa mitaji ya kigeni katika sekta mbalimbali ikiwemo huduma za fedha, elimu, utamaduni na matibabu, na kutoa hadhi ya raia kwa makampuni ya kigeni

    Inatarajiwa kuwa ufunguaji mlango wa duru mpya utakaoanzishwa na China utatoa nafasi kubwa zaidi kwa kampuni za kigeni kustawi nchini China. Iwapo zinafuata sheria za China na kufanya ushindani wenye usawa, kampuni hizo zitapata fursa nyingi zaidi nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako