• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa uwekezaji na ushirikiano wa utalii kati ya China na Kenya wafanyika mjini Beijing

  (GMT+08:00) 2018-04-12 19:29:32

  Mkutano wa uwekezaji na ushirikiano wa utalii kati ya China na Kenya kuhusu "Ukanda Mmoja na Njia Moja" umefanyika mjini Beijing.

  Mkutano huo umehudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya utalii na Wanyamapori ya Kenya, ubalozi wa Kenya nchini China, Kamati ya kitaaluma ya Kuhimiza Uchumi na Biashara ya China na Afrika na Kampuni ya njia ya Hariri ya China. Mkuu wa Kamati ya kitaaluma ya Kuhimiza Uchumi na Biashara ya China na Afrika Bw. Liu Junjie amesema, watu wa nchi hizo mbili wamepata mafanikio makubwa katika sekta za uchumi, biashara, utamaduni na mawasiliano yasiyo ya kiserikali. Katika mchakato muhimu wa kuhimiza ujenzi wa"Ukanda Mmoja na Njia Moja", anatumai kuwa China na Kenya zinaweza kuendeleza ushirikiano wa uwekezaji na utalii.

  Balozi wa Kenya nchini China Bw. Michael Kinyanjui Mukiri ameeleza matumaini mazuri na maeneo mapya yatakayofanyiwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili chini ya mpango wa " Ukanda Mmoja na Njia Moja ".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako