• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Ada za kuegesha magari zapandishwa katika uwanja wa JKIA NAIROBI

  (GMT+08:00) 2018-04-12 19:47:03

  Halmashauri ya viwanja vya ndege nchini Kenya imeongeza ada ya kuegesha magari katika uwanja ya kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

  Hatua inalenga kuongeza ukusanyaji wa ushuru kwa ajili ya kufidia gharama kubwa ya upanuzi wa uwanja huo.

  Ada hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu, kwa mujibu wa notisi ya watoaji huduma za kuegesha magari katika uwanja huo KAPS.

  Kwa bei za sasa,kuegesha magari kwa mda wa dakika 20 ni shilingi 100,na mda wa dakika 20 hadi 40 watatozwa shilingi 250.

  Uegeshaji magari wa dakika 40 hadi saa moja utatozwa shilingi 350 na kutoka saa moja hadi 2 watatozwa shilingi 500.

  Wahudumu wa Taxi wamelalamikia ada hizo wakisema zimepanda sana na zitaathiri biashara zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako