• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia:Ethiopia kuanzisha kiwanda cha kutengeza ndege

  (GMT+08:00) 2018-04-12 19:47:28

  Afisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege za Ethiopian Airlines Tewolde GebreMariam, amesema wamekubaliana na kampuni ya vifaa vya ndege ya Aerosud kushirikiana kuanzisha kiwanda cha kutengeza vifaa vya ndege.

  Tewolde amesema kiwanda hicho kitabuni fursa nyingi za ajira kwa vijana waliohitimu kwenye masomo ya uhandisi pamoja na kuipatia serikali mapato.

  Vifaa vitakavyototengezwa katika kiwanda hicho Ethiopia vitauzwa kwa ndege aina ya Boeing na Airbus kwa mashirika mbali mbali duniani.

  Kiwanda hicho kitajengwa katika uwanja wa kimataifa wa Bole nje ya jiji la Addis Ababa.

  Ethiopia imekuwa na ndoto ya zaidi ya miaka 15 ya kuweka kiwanda hichi pamoja kuongoza katia huduma za safari za ndege barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako