• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Mabasi ya mwendo kasi sasa kuhudumu Dareslaam yote

  (GMT+08:00) 2018-04-12 19:48:33

  Utengenezaji wa I wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) maarufu mwendo kasi kwenda Mbagala na Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam, umepangwa kuanza mwaka huu.

  Aidha, usanifu wa ujenzi wa miundombinu ya Dart, utakaohusisha barabara za Sam Nujoma, Bagamoyo, Bibi Titi na Ali Hassan Mwinyi zenye urefu wa kilometa 25.9, pia unaanza mwaka huu wa fedha.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema ujenzi huo utakwenda pamoja na utekelezaji mpango kazi wa fidia ya makazi kwa waathirika wa mradi wa awamu ya pili na tatu na kulipa fidia kwa ajili ya mradi wa awamu zote.

  Aidha ujenzi wa miundombinu hiyo ya Mbagala na Gongo la Mboto, umepangwa kuanza Desemba mwaka huu chini ya awamu ya pili na tatu.

  Ujenzi awamu ya pili (Mbagala) utahusisha barabara za Kilwa, Kawawa, Sokoine, Gerezani, Bandari na Chang'ombe zenye urefu wa kilometa 20.3 na ujenzi utaanza baada ya kumpata mkandarasi.

  Mradi huo utatekelezwa kupitia mkopo wa dola za Marekani milioni 141.71 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika. Kwa upande wa awamu ya tatu ya ujenzi (kwenda Gongo la Mboto), utahusisha barabara za Nyerere, Uhuru, Bibi Titi, Azikiwe, Shaurimoyo, Lindi na Maktaba zenye urefu wa kilometa 23.6 kwa mkopo wa dola za Marekani milioni 148.2 kutoka Benki ya Dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako