• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Madaktari na walimu kunufaika pakubwa kwenye bajeti ndogo

  (GMT+08:00) 2018-04-12 19:48:54

  Wizara ya fedha nchini Kenya itatoa shilingi bilioni 18.1 kwa madaktari na shilingi bilioni 16.3 kwa tume ya walimu kwenye bajeti ndogo ya kujaliza mapengo ya sekta zilizokosa maendeleo.

  Hii ni kufuatia agizo la rais Uhuru Kenyatta la kuzingatia ajenda kuu za maendeleo katika awamu yake ya pili ya uongozi.

  Walimu na madktari waliokuwa na malalamishi ya nyongeza ya marupurupu sasa huenda wakapewa fedha zao.

  Hazina kuu ya fedha imetupilia mbali bajeti ya maendeleo ya sekta nyingine na kuzingatia mahitaji ya kitaifa kwa wakati huu.

  Mwaka jana Rais Uhuru Kenyatta alitangaza azimio la kuimarisha sekta ya afya,kilimo,viwanda na usalama wa chakula.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako