• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yasema matokeo ya uchunguzi wa sumu uliofanywa na OPCW hayaaminiki

    (GMT+08:00) 2018-04-13 08:30:25

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Russia Bi. Maria Zakharova amesema matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Shirika la kupiga marufuku silaha za kikemikali OPCW kuhusu sumu aliyowekewa jasusi wa zamani wa Russia nchini Uingereza, hayaaminiki. Kauli hiyo imekuja baada ya OPCW kutangaza kuwa uchunguzi uliomalizika umethibitisha matokeo yaliyotangazwa awali na Uingereza kuwa sumu iliyotumiwa kwenye tukio hilo ni sumu ya neva ya Russia aina ya "Novichok". Bi. Zakharova amesema kutolewa kwa matokeo hayo ni uchokozi mwingine wa Uingereza dhidi ya Russia chini ya ushiriki wa idara yake ya ujasusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako