• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wazitaka nchi za Afrika kuhakikisha gesi ya kupikia inawafikia wananchi

    (GMT+08:00) 2018-04-13 09:02:07

    Katibu mkuu wa mkataba wa umoja wa mataifa wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa Bibi Patricia Espinosa amezitaka serikali za nchi za Afrika kuhakikisha gesi ya kupikia inawafikia watu maskini ili kubadilisha matumizi ya nishati za viumbe.

    Bibi Espinosa amezitaka serikali za nchi za Afrika kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuwa sekta nyingi kama vile kilimo, utalii na maji ambazo zina msaada mkubwa kwa watu wengi, zinakaribia kuanguka kutokana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Akiongea kwenye mkutano wa 10 wa baraza la kaboni Afrika, Bibi Espinosa amesema nchi nyingi za Afrika zimepunguza matumizi ya nishati zinazochafua mazingira kutokana na matumizi ya teknolojia za nishati safi, lakini zinatakiwa kufanya juhudi zaidi.

    Waziri wa Mazingira na Misitu wa Kenya Bw Keriako Tobiko amesema Kenya inaendelea kupiga hatua kwenye matumizi ya nishati safi, na sasa kuna miradi 40 ambayo iko njiani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako