• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshindi wa tuzo ya Nobel amesema uamuzi wa Marekani kuitoza China ushuru mkubwa wa forodha unavuruga kanuni za biashara ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-04-13 09:02:52

    Mshindi wa tuzo ya Nobel ya uchumi Bw. Joseph Stiglitz amesema uamuzi wa upande mmoja wa Marekani kutoza ushuru mkubwa wa forodha dhidi ya bidhaa za China unavuruga utaratibu wa biashara wa pande nyingi, ambao umetoa mchango mkubwa kwenye ongezeko la uchumi wa dunia.

    Akiongea jana kwenye mjadala kuhusu mambo ya uchumi kwenye mkutano uliofanyika katika chuo Kikuu cha Harvard, Bw. Stiglitz amesema njia aliyotumia Rais Trump kukabiliana na mgogoro wa biashara na China sio nzuri. Bw. Stiglitz amesema ni ujinga kufikiri kuwa anaweza kuondoa pengo la biashara kwa siku moja.

    Bw. Stiglitz pia ameonyesha wasiwasi wake kuhusu malalamiko ya Rais Trump kuwa WTO inaionea Marekani, na kuzuia uteuzi wa majaji wapya wa jopo lenye wajumbe saba, linaloshughulikia utatuzi wa migogoro ya biashara. Kwa sasa jopo hilo lina wajumbe wanne tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako