• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yasema mradi wa SGR kutoathiri wanyamapori wa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-04-13 10:01:48

    Kampuni ya China inayorefusha reli ya SGR nchini Kenya kutoka Nairobi hadi Naivasha imesema mradi huo hautaathiri mazingira ya wanyamapori.

    Msemaji wa ofisi ya SGR ya Kenya Bw. Steve Zhao amesema, ujenzi huo utakaopita kwenye mbuga za taifa, utazingatia masuala ya kimazingira kwa wakati wote. Bw. Zhao pia amesema, ujenzi wa daraja kubwa katika mbuga ya taifa ya Nairobi umeidhinishwa na mamlaka ya wanyamapori ya Kenya KWS.

    Pia amesema hivi sasa mradi huo unaotarajiwa kumalizika mwaka kesho, utasaidia miji ya ndani ya Kenya kuvutia biashara na uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako