• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yapitisha makubaliano ya eneo la biashara huria barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-04-13 10:03:33

    Baraza la mawaziri la Rwanda limepitisha mswada wa sheria inayoidhinisha Eneo la biashara huria barani Afrika AfCFTA.

    Baraza hilo pia limepitisha itifaki kuhusu biashara ya bidhaa na huduma, pamoja na utaratibu wa kusuluhisha migogoro uliosainiwa mwezi Machi mjini Kigali, Rwanda.

    Makubaliano ya eneo la biashara huria barani Afrika yanayolenga kuongeza biashara kati ya nchi za Afrika, yamesainiwa na zaidi ya nchi 44 kwenye Mkutano wa 10 wa viongozi wa nchi na serikali za Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Kigali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako