• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa wazitaka nchi zinazoendelea kujumuisha mabadiliko ya hali ya hewa kwenye mipango miji

  (GMT+08:00) 2018-04-13 17:33:27

  Shirika la Mpango wa Makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat limetoa wito kwa nchi zinazoendelea kujumuisha mabadiliko ya hali ya hewa kwenye mipango miji.

  Akihutubia mkutano wa 10 wa uchafuzi wa hewa barani Afrika unaofanyika Nairobi, Kenya, mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Maimunah Mohamed Sharif amesema kuna haja ya kuendeleza mipango miji endelevu ambayo inachochea muunganiko na miundombinu ambayo inaendana na juhudi za kupunguza utoaji wa hewa chafu.

  Bi. Sharif amesema, kutokana na kuongezeka kwa uhamiaji wa watu katika maeneo ya miji, kuna uwezekano kuwa utoaji wa hewa chafu unaweza kuongezeka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako