• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Ulaya kuisaidia Ugiriki na nchi nyingine kukabiliana na suala la wakimbizi

  (GMT+08:00) 2018-04-13 17:56:10

  Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia uhamiaji, mambo ya ndani, na mambo ya raia Bw. Dimitris Avramopoulos, amesema Umoja wa Ulaya utaendelea kuisaidia Ugiriki, Italia na nchi nyingine zinazokabiliwa na suala la wakimbizi.

  Bw. Avramopoulos amesema hayo jana alipotembelea kambi ya wakimbizi ya Titsona, kaskazini ya mji wa Athens. Amesema changamoto zinazoikabili Ugiriki ni changamoto za pamoja zinazoukabili Umoja wa Ulaya, na kamati ya Umoja wa Ulaya iko tayari kuiunga mkono Ugiriki.

  Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, kuanzia mwaka 2015 hadi sasa, zaidi ya wakimbizi milioni moja walifika nchini Ugiriki kutoka Uturuki, na mpaka sasa bado kuna zaidi ya wakimbizi elfu 60 wanaoishi nchini Ugiriki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako