• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la majini la Libya lawaokoa wahamiaji 137 haramu

    (GMT+08:00) 2018-04-13 18:10:05

    Jeshi la majini la Libya limewaokoa wahamiaji 137 haramu baada ya boti mbili walizokuwa wakisafiria kupata hitilafu kwenye pwani ya mji wa Zawiya, magharibi mwa nchi hiyo.

    Msemaji wa jeshi hilo Ayoub Qassem amesema wahamiaji waliookolewa ni pamoja na raia mmoja wa Syria, na wengine wanatoka Afrika, wakiwemo wanawake 19 na watoto wanne. Baada ya kupata huduma za matibabu kwenye kituo cha jeshi la majini mjini Tripoli, wahamiaji hao wamepelekwa ofisi ya kupambana na wahamiaji haramu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako