• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Papua New Guinea

    (GMT+08:00) 2018-04-13 19:17:54

    Mumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Papua New Guinea Rimbink Pato ambaye yupo ziarani hapa China.

    Wang amesema, China inaunga mkono Papua New Guinea kwa kufanya mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasific (APEC), na iko tayari kuimarisha uratibu na ushirikiano kati ya pande hizo mbili chini ya mfumo wa APEC. Wang pia amesema, rais Xi Jinping wa China atafanya ziara nchini Papua New Guinea mwezi Novemba mwaka huu ambapo pia atahudhuria mkutano wa wakuu wa APEC.

    Kwa upande wake, Bw. Pato amesema Papua New Guinea iko tayari kushirikiana na China ili kuboresha ushirikiano katika pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, ili kulifanya kuwa mfano wa kuigwa katika kanda ya Pasific.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako