• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 16 wa mawasiliano ya watu wenye vipaji wa kimataifa wa China wafanyika huko Shenzhen

  (GMT+08:00) 2018-04-14 17:33:39

  Mkutano wa 16 wa mawasiliano ya watu wenye vipaji wa kimataifa wa China leo umefanyika huko Shenzhen. Mkutano huo ulikuwa na mada iliyolenga ya kukusanya mawazo mbalimbali ya watu duniani na kuhimiza maendeleo ya pamoja, na ulikwa na sehemu 18 zikiwemo kongamano la viongozi, majadiliano kuhusu maonyesho, ajira za watu wenye vipaji, kufanya ushirikiano wa miradi, mikutano ya wataalamu na mashindano ya uvumbuzi mpya wa Shenzhen.

  Naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya wataalamu wa nchi za nje ya kitaifa ya China Bw. Zhang Jianguo alisema katika ufunguzi kuwa, China itatekeleza kwa pande zote hatua za kurahisisha leseni za kufanya kazi nchini China kwa wageni na viza kwa wataalamu wa kigeni, kuanzisha majukwaa mengi zaidi ya ushirikiano wa sayansi na tekenolojia ya kimataifa, kuunda ubora wenye nguvu ya mashindano ya kimataifa wa mfumo wa watu wenye vipaji, kuinua kiwango cha ubora wa huduma kwa kufanya kazi nchini China kwa wageni, na kuanzisha mazingira mazuri kwa uvumbuzi wa watu wenye vipaji wa kigeni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako