• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ateua kamanda mpya wa MONUSCO

    (GMT+08:00) 2018-04-14 18:15:37

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemteua Bw. Elias Rodrigues Martins Filho wa Brazil kuwa kamanda wa vikosi vya umoja huo vinavyolinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO).

    Luteni Jenerali Filho anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Derrick Mbuyiselo Mgwebi wa Afrika Kusini ambaye alikamilisha majukumu yake januari 31 mwaka huu, ambaye pia katibu mkuu huyo amemshukuru kwa uongozi wake uliotukuka.

    Filho amelitumikia jeshi la Brazil katika nyadhifa tofauti kwa kipindi cha miaka 35, ambapo kwa sasa alikuwa anahudumu katika nafasi ya mkuu wa Ofisi za mashirika ya kimataifa kwenye wizara ya Ulinzi ya Brazil tangu mwaka 2017, na ana uzoefu wa kushughulikia masuala ya ulinzi wa amani kwani aliwahi kuhudumu katika nafasi ya afisa mipango wa Idara ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kutunza amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako