• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wa Afrika wazindua mpango wa utekelezaji wa kutimiza malengo ya umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-04-14 18:20:23
    Watunza mazingira kutoka barani Afrika jana wamezindua utekelezaji wa mpango wa kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Watunga sera hao kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambao wamemaliza mkutano wao wa siku mbili waliainisha mapendekezo ya njia zakukabiliana na Visababishi vya kitaifa vilivyogundulika(NDC) ambayo wamesema yakitekelezwa mchango wa bara katika kupunguza uchafuzi wa mazingira duniani.

    Washiriki wa mkutano huo wa majadiliano walisema wanalenga kutekeleza mapendekezo yao kwa kutoa vipaumbele katika kufadhili pendekezo hilo, mabadilishano ya teknolojia na kuzijengea uwezo jamii.

    Walikubaliana kuinua kiwango cha matumizi ya sayansi na teknolojia kwa kuanzisha uwekezaji katika hali ya hewa barani Afrika, kwa kuhamisha teknolojia baina ya jamii ili kuzisaidia jamii hizo na kulinda miundo mbinu dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia makazi amezitaka serikali za nchi mbalimbali kujitoa na kuruhusu utekelezaji wa sera za kimataifa za amabadiliko ya hali ya hewa, huku akiahidi kuwa shirika lake litazisaidia nchi zinazoendelea kupanga mikakati endelevu kwenye miji yake yenye kushirikisha jinsia zote katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako