• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kamanda mwandamizi wa Alshabab ajisalimisha serikali

  (GMT+08:00) 2018-04-15 18:20:11

  Kamanda mmoja mwandamizi wa kundi la Alshabab jana amejisalimisha kwenye vikosi vya usalama vya Somalia katika mji wa Bula-hawo uliopo eneo la kusini mwa Somalia la Gedo.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na afisa usalama kutoka vikosi vya Somalia vya eneo hilo Ali Hassan Abdi, vikosi vya usalama vya Somalia vinakaribisha vikundi vyote vya wapiganaji au makamanda ambao wataamua kuasi vikundi vyao na kukubali wito wa amani uliotangazwa na serikali.

  Akitolea mfano wa kamanda mwandamizi aitwaye Abdihakim Hussein Yusuf ambaye aliamua kuliasi kundi la Al-shabab na kujisalimisha kwenye vikosi vya serikali ya Somali.

  Muasi-Kamanda Abdihakim amivisifu vikosi vya Somalia kwa kumpokea huku akisema kuna wapiganaji wengine ambao pia wanataka kuasi vikundi vyao. Licha ya kuwa mpaka sasa hakuna kundi lolote lililozungumza tangu serikali ianze kuwapokea waasi walioasi vikundi vyao.

  Katika hatua nyingine vikosi vya Umoja wa Afrika vinavyolinda usalama nchini Somalia vimenza utekelezaji wa mpango wa kupunguza taratibu wanajeshi wake katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

  Akizungumzia sula hilo Naibu kiongozi wa mwakilishi wa mwenyekiti wa baraza la AU nchini Somalia, Bwana Simon Mulongo amesema zoezi hilo linatekelezwa kwa utaratibu maalum na kwa kufuata azimio la Umoja wa Mataifa la kupunguza wanajeshi wanaohudumu Somalia.

  Zoezi hilo linafanyika sambamba na hatua ya kuhamishia wajibu wa ulinzi kwa vikosi vya Somalia kama ilivyoamriwa na Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako