• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashambulizi dhidi ya Syria yalaaniwa vikali na pande mbalimbali kote duniani

    (GMT+08:00) 2018-04-15 18:30:00

    Mashambulizi yaliyofanywa na Marekani pamoja na washirika wake nchini Syria kwa madai ya kuangamiza hifadi za silaha za kikemikali nchini Syria yamepokelewa kwa masikitiko na yamezua hofu kubwa duniani, na kusababisha viongozi wengi wa kisiasa kutoa wito kwa pande zinazohusika kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kuzuia kuongezeka kwa mgogoro.

    Mashambulizi yaliyoanzishwa na Marekani pamoja na washirika wake ambao ni Uingereza na Ufaransa mapema siku ya jumamosi, yalitokana na ripoti iliyodai kulikuwa na matumizi ya silaha za kikemikali katika eneo la Douma lililoko jirani na mji mkuu wa Damascus.

    Serikali ya Syria imekanusha vikali madai hayo, na kutoa wito kwa shirika la kuzuia matumizi ya silaha za kikemikali (OPCW) kuendesha zoezi la uchunguzi. Lakini hata hivyo, mataifa matatu yalianza kushambulia siku ambayo ujumbe kwa ajili zoezi la uchunguzi ulipowasili mjini Damascus.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Bi. Hua Chunying jana alizitaka pande zinazohusika kurejea kwenye mfumo wa sheria ya kimataifa na kutatua suala la Syria kupitia majadiliano na mapatano.

    Katika hatua nyingine Bi. Hua amesema China inapinga matumizi ya mabavu katika mahusiano ya kimataifa na inatoa wito wa kuheshimu uhuru wa nchi nyingine, uhuru na misimamo ya nchi nyingine.

    Naye kiongozi wa Chama kiuu cha upinzani cha nchini Uingereza 'Labor Party' bwana Jeremy Corbyn amelielezea jambo hilo kuwa ni kitendo cha uvunjaji wa sheria, na amesema mabomu hayawezi kuokoa maisha au kuleta amani.

    Rais wa Finland Sauli Niinisto amesema mashambulizi hayo hayatatatua chochote, isipokuwa yamelenga zaidi kuadhibu.

    Ujumbe mwingine wa kulaani vikali mashambulio hayo umetolewa katika taarifa ya Wizara ya mambo ya nje ya Belarus ambayo imesema matumizi ya silaha za maangamizi hayatakiwi kuvumiliwa kwa kuwa yanasababisha madhara zaidi.

    Wengine waliotoa makaripio kuhusu mashambulizi hayo ni Wizara ya mambo ya nje ya Tunisia, Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Pakistan Bw. Mohammad Faisal, Rais wa Brazil Michel Temer, na Rais wa Argentina Maurico Macri.

    Katika hatua nyingine, azimio lililopendekezwa na Russia dhidi ya mashambulizi ya nchini Syria yaliyofanywa na Marekani na washirika wake limeshindwa kupitishwa na wajumbe wa baraza la usalama.

    Imeshindwa baada ya baadhi ya wajumbe kujitoa, wengine wakilipinga azimio hilo, na likipigiwa kura ya kupitishwa na nchi tatu ambazo ni Russia yenyewe, Bolivia na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako